Leo Tarehe 05/09/2024 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi (WUMU) Dkt Habiba Hassan Omar ametembelea Shirika la Bandari na kufanya kikao na Uongozi wa Shirika na kusisitiza masuala mbali mbali ikiwemo kufanya kazi kwa mashirikiano ili kutimiza dhamira iliyowekwa kuweza kuyafikia malengo yakimaendeleo ya Shirika.