Shirika la Bandari Zanzibar limeendeleza utaratibu wake wa kila mwisho wa mwezi kwa kufanya kikao na wadau wake wa sekta ya Bandari ili kutoa taarifa juu ya shughuli za shirika na kupokea taarifa juu ya changamoto zilizopo kuandaa mikakati mbali mbali ili shirika liweze kutatua changamoto hizo kwa lengo la kuongeza ufanisi katika sekta ya Bandari.
Kikao hicho kimefanyika tarehe 27/08/2024 katika ukumbi wa Mikutano ZURA Maisara, Zanzibar, ikijumuisha ZPC, muendeshaji wa Bandari ya Malindi (ZMT), muwekezaji wa Bandari ya Fumba (FP), wamiliki wa meli za ndani na kimataifa, wakala wa forodha, wamiliki wa meli za majahazi pamoja na wafanya biashara.