Bodi ya Wakurugenzi na uongozi wa Shirika la Bandari (ZPC) umefanya mkutano na bodi pamoja na uongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Siku ya Jumanne Tarehe 20/08/2024 katika makao Makuu ya TPA Dar-es-Salaam, Tanzania.
Madhumuni ya mkutano huo ni kujadili maeneo ya mashirikiano baina ya Mamlaka ya Bandari TPA na Shirika la Bandari Zanzibar ZP, fursa za uwekezaji na biashara baina ya Bandari hizo Mbili 2, Miradi ya mashirikano katika sekta ya Bandari baina ya Zanzibar na Tanzania Bara na utatuzi wa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara kwenye usafirishaji.