Shirika la Bandari (ZPC) ikishirikiana na Taasisi ya Tony Blair Institute (TBI) imekamilisha ripoti ya maandalizi ya stadi maalum ya maboresho ya Bandari za Zanzibar (Zanazibar Port Improvement Charter).
Baada ya kukamilika kwa ripoti hiyo, ZPC imeandaa warsha maalum kwa siku tatu (3) na wadau wa sekta ya Bandari ili kuthibitisha uchunguzi wa ripoti hiyo na kupata maoni kutoka kwa wadau.