Makabidhiano ya vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar amehudhuria makabidhiano ya vyeti kwa wanafunzi waliomaliza mafunzo ya uendeshaji wa vifaa vya kupakia, kushusha na kupanga Makontena katika Bandari ya Malindi ( Reach stacker, Mobile Crane) inayoendeshwa na kampuni ya Zanzibar Multipurpose Terminal (ZMT).

Jumla  ya wanafunzi 41 wamepata mafunzo hayo 18 wakiwa waajiriwa wapya na 23 walobaki ni wale waliotoka Shirika la Bandari  (ZPC).

ZMT wametimiza ahadi yakimkataba ya kuongeza ujuzi kwa wafanyakazi waliopo na kuajiri wafanyakazi wapya ili kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika shughuli za Operesheni za Bandari.