Upepo Mkali wa Kimbunga Hidaya

Baada ya taarifa kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) kuonesha hali ya mwenendo wa upepo mkali wa Kimbunga Hidaya kuimarika, Shirika la Bandari Zanzibar linawataarifu wadau na wananchi kwa ujumla kuwa kuanzia leo tarehe 06/05/2024 huduma za meli, abiria na mizigo katika Bandari zake zote za Unguja na Pemba zimerejea Rasmi.