WIZARA YA UJENZI YATILIANA SAINI UJENZI WA BANDARI KAVU YA USHUSHAJI NA UPAKIAJI WA MAKONTENA FUMBA

Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar kupitia shirika la bandari imetiliana saini na Fumba Inland Container Deport Limited kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu (ICD) katika eneo la Fumba.

Mkataba huo kwa niaba ya wizara umesainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Ndugu Nahat Mohamed Mahafoudh na kwa upande wa Kampuni ya Fumba Inland Contaner Deport Limited umewakilishwa na Ngugu Twalib Khamis.

Akizungumza mara baada ya kuwekwa saini kwa mkataba huo Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed amepongeza jitihada zilizochukuliwa na wadau wa taasisi mbali mbali  kwa kusimamia kwa karibu kukamilika kwa taratibu za kuanza ujenzi wa bandari hiyo ya kushushia na kupakia makontena.

Waziri Dk. Khalid amesema kukamilika kwa ujenzi wa bandari hiyo na kuanza kutumika kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondosha changamoto ya msongamano wa ushushaji wa makontena katika bandari ya Malindi.

 

Pia, Mhe. Waziri kukamilika kwa banadari hiyo ya kushushia makotena kutapelekea kuondosha changamoto ya usafirishaji wa makontena yaliokuwepo Mombasa hatimae kushushwa moja kwa moja katika bandari ya Fumba ndani ya Kipindi cha muda mfupi.

Aidha, Dk. Khalid amewahakikishia wajenzi wa bandari ya Fumba kuwa, Wizara kwa kushirkiakiana na Shirika la Bandari watatoa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha ujenzi unafanikiwa kwa haraka ili kuwaondoshea changamoto wananchi wa Zanzibar hasa katika upatikanaji wa bidhaa kwa bei nafuu.

Nae muwakilishi kutoka Fumba Inland Container Deport Limited Ndugu Twalib Khamis ameipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ujasiri wake katika kuchukua hatua za haaraka za kupunguza tatizo la msongamoano wa meli na mizigo katika bandari ya Malindi.

Ngugu Twalib Khamis ameihakikishia Serikali kuwa, kamapuni yao ina uwezo mkubwa wa kuifanya kazi hiyo kutokana na uzoefu waliokuwa nao na watahakikisha kazi inakamilika kwa muda mfupi ulio ndani ya makubaliano ya Mkataba.

“Tutahakikisha kazi hii inakamilika kwa wakati na meli ya kwanza itanza kushusha makotena mwezi Agosti ndani ya wiki ya kwanza” Alisema Ndugu Twalib Khamis

Imetolewa na Kitengo cha Habari (WUMU).
Mei 10, 2023.